Pages

Tuesday, August 26, 2014

HII NDIO JET YA DAVIDO


davido jet3
Mwimbaji  Davido wa Nigeria amethibitisha kuwa mbali na kuwa mtoto wa bilionea lakini muziki unamlipa kwa kiasi cha kumuwezesha kumiliki private Jet yake.
Kama wewe unamfollow Davido kwenye Instagram yake bila shaka utakuwa shahidi kuwa ‘Skelewu’ hit maker anapiga show nyingi sana sababu post zake nyingi huwa ni kuhusu safari za show.
davido jet
Weekend iliyopita alipost picha akiwa kwenye private Jet hiyo kabla ya safari ya kuelekea Togo kwenye show nyingine.
Davido Jet4

Monday, August 25, 2014

TAZAMA PICHA 20 JINSI KILI TOUR ILIVYOFUNIKA KIGOMA


Wakazi wa mji wa Kigoma na vitongoji vyake wakiwa katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika, Jumamosi Agosti 23, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Amini akitoa burudani katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma Jumamosi Agosti 23, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ben Pol akitoa burudani katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma Jumamosi Agosti 23, 2014. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.