Wakazi
wa mkoa wa Kigoma jana walijiwekea historia ya pekee kwa kujitokeza kwa
wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,lililofanyika jana kwenye
uwanja wa Lake Tanganyika,hii ikiwa ni mara ya kwanza tamasha hilo
kufanyika mkoani humo,ambao wakazi wake wengi wanaishi kwa kutegemea
kilimo.Pichani ni Msanii wa Bongofleva TID a.k.a Mnyama Unyamani
akiwatumbuiza wakazi wa Kigoma mapema jana usiku.
Wakali
wengine mahili wa muziki wa Hip hop Bongo,Mwana FA pamoja na AY
wakiwarusha vilivyo maelfu ya watazamaji waliojitokeza usiku wa kuamkia
leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Lake
Tanganyika.
Pichani
kulia ni mmoja wa Madj wakali ndani ya Clouds FM,Dj Zero akikamua ngoma
mbalimbali kwa ajili ya kuwaburudisha wakazi wa Kigoma,shoto kwake ni
Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha XXL,B Dozen akifuatilia kwa
makini yaliyokuwa yakijiri jukwaani-
Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliojotokeza kwenye tamasha la Fiesta 2013.
Msanii
Ommy Dimpo a.k.a Tupogo akiimba wimbo wake mpya wa Tupogo
aliomshirikisha mwanamuziiki nguli kutoka nchini Nigeria,J-Martins mbele
ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha
la Fiesta 2013.
Wasanii mahiri kutoka kundi la Wanaume Family,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa la Fiseta kwa pamoja.
Msanii
mmojawapo kutoka kundi la Manzese Crew,ajulikanae kwa jina la Madee
akiimba wimbo wake wa Nani kaiba pombe yake,huku sehemu ya umati
ikishangilia kwa shangwe.
Sehemu
ya umati wa watu ukifuatilia yaliyokuwa yakijiri usiku wa kumakia leo
kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkoani
Kigoma.Picha zote na michuzijr
No comments:
Post a Comment