Pages

Monday, October 28, 2013

KIGOMA: KILI MUSIC TOUR 2013.


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Izzo Bizness akiwapagawisha washabiki katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
 Umati wa mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha la Kili Music Tour, wakifuatilia onyesho hilo lililofanyioka kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
 Baadhi ya wasanii wa muziki nchini wakiwa pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ akifanya yake katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika Kigoma.
 Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Joseph Haule ‘Profesa Jay’ akitumbuiza katika tamasha la Kili Music Tour Kigoma.
 Diamond akiongoza wasanii wenzake Mwasiti, Linex na Recho katika nyimbo ya ‘Leka Dutigite’ na kuwaamsha mashabiki waliofurika uwanja wa Lake Tanganyika katika tamasha la Kili Music Tour, mjini Kigoma.
 Msanii wa muziki nchini Lady Jaydee ‘Jide’ akitumbuiza kwenye tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wLake Tanganyika mjini Kigoma.

FIESTA 2013 MKOANI KIGOMA NOMA SANAAAAAA


 Wakazi wa mkoa wa Kigoma jana walijiwekea historia ya pekee kwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,lililofanyika jana kwenye uwanja wa Lake Tanganyika,hii ikiwa ni mara ya kwanza tamasha hilo kufanyika mkoani humo,ambao wakazi wake wengi wanaishi kwa kutegemea kilimo.Pichani ni Msanii wa Bongofleva TID a.k.a Mnyama Unyamani akiwatumbuiza wakazi wa Kigoma mapema jana usiku.
 Wakali wengine mahili wa muziki wa Hip hop Bongo,Mwana FA pamoja na AY wakiwarusha vilivyo maelfu ya watazamaji waliojitokeza usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
 Pichani kulia ni mmoja wa Madj wakali ndani ya Clouds FM,Dj Zero akikamua ngoma mbalimbali kwa ajili ya kuwaburudisha wakazi wa Kigoma,shoto kwake ni Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha XXL,B Dozen akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri jukwaani-
 Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliojotokeza kwenye tamasha la Fiesta 2013.
 Msanii Ommy Dimpo a.k.a Tupogo akiimba wimbo wake mpya wa Tupogo aliomshirikisha mwanamuziiki nguli kutoka nchini Nigeria,J-Martins mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2013.
 Wasanii mahiri kutoka kundi la Wanaume Family,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa la Fiseta kwa pamoja.
 Sehemu ya umati wa watu.
 Msanii mmojawapo kutoka kundi la Manzese Crew,ajulikanae kwa jina la Madee akiimba wimbo wake wa Nani kaiba pombe yake,huku sehemu ya umati ikishangilia kwa shangwe.
 Sehemu ya umati wa watu ukifuatilia yaliyokuwa yakijiri usiku wa kumakia leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkoani Kigoma.Picha zote na michuzijr